Dodoma FM

Majengo waeleza kunufaika na mikopo

27 November 2023, 2:11 pm

Picha ni mmoja wa wafanyabiashara katika soko la Majengo akiongea na Dodoma Tv . Picha na Khadija Ibrahim.

Uwepo wa Taasisi za kifedha zinazojihusisha na utoaji wa mikoo kwa wajasiliamali imechangia kukuza biashara zao na kupata kipato cha kuendesha familia.

Na Khadija Ibrahim.

Wafanyabiashara katika soko kuu la majengo Jijini Dodoma wameeleza kunufaika kiuchumi kutokana na mikopo inayotolewa sokoni hapo kupitia taasisi mbalimbali za kifedha.

Dodoma tv imefika katika soko la majengo na kuzungumza na baadhi ya wafanyabiashara hao ambapo wamezitaja faida wanazozipata kutokana na uwepo wa fursa za mikoo.

Picha ni mmoja wa wafanyabiashara katika soko la Majengo akiongea na Dodoma Tv . Picha na Khadija Ibrahim.

Wamesema kuwa kupitia fursa hiyo imewasaidia kukuza biashara zao huku wakibainisha baadhi ya mambo ya kuboresha katika suala hilo.

Sauti za wafanyabiashara.

Mwenyekiti wa soko kuu la majengo jijini Dodoma Bw. Godson Rwegazama amefafanua namna wafanyabiashara katika soko hilo wanavyochangamikia fursa ya mikopo kuendesha biashara zao.

Sauti ya Bw. Godson Rwegazama.