Dodoma FM

Operesheni ya kukamata wezi wa vyuma yaendelea Mpwapwa

26 April 2023, 3:01 pm

Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa Bi. Sophia Kizigo akizungumza na wakazi wa kijiji cha Berege. Fred Cheti.

Katika oparesheni hiyo ametoa muda kwa wale wote walio uziwa vyuma hivyo bila kujua wavikabidhi kwa watendaji.

Na Fred Cheti.

Mkuu wa Wilaya ya Mpwampwa Mhe.Sophia Kizigo amesema wanaendelea na operesheni maalum ya kukamata watu wanaoiba vyuma vilivyofungwa kwenye minara ya kupitisha nyaya za umeme katika mradi wa reli ya kisasa ya SGR.

Kwa mujibu wa Kizigo hadi sasa jumla ya watu nane katika Kata ya Berege, kijiji cha Berege ambako mradi wa SGR umepita wanashikiliwa kwa tuhuma za kujihusisha na wizi wa vyuma hivyo na kisha kuuza kwa wanunuzi wa vyuma chakavu.

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Mpwapwa.
Wakazi wa Berege Mpwapwa wakifuatilia mkutano huo ,

Sambamba na hilo Wataalam kutoka Tanesco nao wameendelea kutoa elimu kwa wananchi wa kijiji cha Berege katika kata ya Berege kuhusu utambuzi wa vyuma vilivyoibwa katika mradi wa njia ya umeme ya SGR, na masuala mengine mtambuka.

Sauti ya mtaalam kutoka Tanesco