Dodoma FM

Halmashauri ya jiji Dodoma kugawa viwanja 1,035 kama fidia

3 July 2023, 2:15 pm

Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Bwana John Kayombo akizungumza na baadhi ya wananchi wenye changamoto za viwanja pamoja na baadhi ya watendaji wa ardhi wa jiji. Picha na Fred Cheti.

Mwaka wa fedha ujao 2023/2024 halmashauri inatarajia  kupima takribani viwanja 6,000.

Na Fred Cheti.

Halmashauri ya jiji la Dodoma inatarajia kugawa jumla ya viwanja 1,035 kwa kufidia na kuwapunguzia  wananchi wanaodai viwanja takribani viwanja 3,995 eneo la Nala.

Hayo yameelezwa na mkurugenzi wa jiji la Dodoma Bwana John Kayombo wakati akizungumza na baadhi ya wananchi wenye changamoto za viwanja pamoja na baadhi ya watendaji wa ardhi wa jiji  pamoja na Waziri wa Ardhi Mh Angelina Mabula ambapo amesema Kamati ya Ugawaji Ardhi imeshakaa na tayari wamekubaliana kugawa viwanja hivyo.

Sauti ya Mkurugenzi wa jiji la Dodoma.
Baadhi ya wananchi wenye changamoto za viwanja pamoja na baadhi ya watendaji wa ardhi wa jiji wakiwa katika mkutano huo. Picha na Fred Cheti.

Aidha mkurugenzi huyo amesema kuwa kwa mwaka wa fedha ujao 2023/2024 halmashauri inatarajia  kupima takribani viwanja 6,000 huku viwanja 2,960 vikitarajiwa kugawiwa wananchi  kwa ajili ya kukamilisha changamoto ya viwanja ambavyo wananchi wanavidai.

Sauti ya Mkurugenzi wa jiji la Dodoma.