Wananchi watakiwa kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya virus vya Ebola
22 May 2026, 17:53

Mtaalamu huyo wa afya ameitaka jamii kwa ujumla kuzingatia elimu inayotolewa na endapo mtu akibainika kutokana na dalili tajwa afikishwe kituo cha afya au hospitali iliyo karibu kwa uchunguzi zaidi.
Na Jerome John.
Wananchi mkoani Dodoma wametakiwa kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya virus vya ugonjwa wa Ebola.
Wito huo umetolewa na Vumilia William kutoka chuo kikuu cha St. John Dodoma akizungumza katika kipindi cha Dodoma live juu ya elimu na namna ya kujikinga na ugonjwa huo pindi akigundulika mtu mwenye maambukizi.
Bi,Vumilia amesema kuwa ingawa Tanzania hakujatolewa taarifa yoyote ya ugonjwa huo ila ni vema jamii kwa ujumla kupata elimu ya namna ya kujikinga na kuzifahamu dalili za ugonjwa huo ambao umetolewa taarifa na shirika la afya Duniani kuwa umesababisha vifo kadhaa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Aidha amebainisha dalili za ugojwa huo kuwa ni mtu kuwa na homa kali,kutapika,kuharisha na mwili kukosa nguvu pamoja na uchovu wa mara kwa mara.
Vile vile ameeleza kuwa tahadhari zinazopaswa kuchukuliwa ni kuto kugusana ,kukumbatiana, au kugusa mwili wa mtu ambaye amefariki dunia kwa ugonjwa huo kwani ugonjwa huo huambukizwa kwa njia ya majimaji.