Dodoma FM

Wakulima watakiwa kufanya machaguo sahihi ya mbegu

29 November 2023, 3:01 pm

Picha ni Taasisi ya kilimo ya utafiti wa kilimo Tanzania TARI iliyopo makutupora jijini Dodoma.Picha na Thadei Tesha.

Mara kadhaa wakulima wameendelea kshauriwa kulima kilimo cha kisasa ikiwa ni pamoja na kufuata kanuni na taratibu ili waweze kupata mavuno bora.

Na Thadei Tesha.
Wakati mamlaka ya hali ya hewa kanda ya kati ikitoa taarifa juu ya uwepo wa mvua wataalamu wa mbegu za kilimo wameendelea kutoa ushauri kwa wakulima juu ya machaguo sahihi ya mbegu kwa ajili ya shughuli za kilimo zinazotarajia kuanza hivi karibuni.

Dodoma Tv imefika makao makuu ya Taasisi ya utafiti wa kilimo Tanzania TARI iliyopo makutupora jijini hapa na kufanya mahojiano maalum na mratibu wa utafiti TARI Makutupora bw. Endolei Salum ambapo hapa anatumia fursa hii kuwataka wakulima kufanya machaguo sahihi ya mbegu wakati wa kilimo.

Aidha Dodoma Tv imefanya mahojiano na mtafiti wa mbegu za mazao ya kilimo cha chakula kutoka TARI MAKUTUPORA Bi Sada Omary hapa anawataka wakulima kuacha kurudia mazao kama mbegu na badala yake kununua mbegu zilizothibitishwa na wataalamu wa mbegu na ubora kutoka TOSCI.