Dodoma FM

Wakazi wa kata ya Handali waaswa kuepuka kupitisha mifugo barabarani

18 October 2021, 11:55 am

Na; Benard Filbert.

Wakazi wa kata ya Handali wilaya ya Chwamwino mkoani Dodoma wameombwa kuepuka kupitisha mifugo kwenye barabara kuepuka uharibifu ambao umekuwa ukitokea.

Hayo yanajiri kufuatia hivi karibuni kukamilika kwa marekebisho ya barabara za ndani katika kata hiyo.
Akizungumza na taswira ya habari Diwani wa kata ya Handali Bwana Aidan Simon Lubeleje amekiri kuwepo kwa baadhi ya wananchi ambao wanapitisha mifugo katika barabara hali inayosababisha kuharibika kwa barabara.

CLIP DIWANI…………………..01

Amesema serikali inatumia gharama kubwa kutengeneza barabara hizo hivyo ni vyema zikatunzwa na sio kulalamika pindi zinapoharibika.

CLIP DIWANI…………………..02

Akizungumzia barabara iliyokamilika hadi hivi sasa katika kata hiyo amesema ni kutoka Handali hadi chanumba ambazo zitasaidia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa uchumi kwa wananchi.

CLIP DIWANI…………………..03

Kukamilika kwa barabara katika kata ya Handali wilaya ya Chamwino itasaidia kukuwa kwa uchumi wa wakazi wa kata hiyo.