Dodoma FM

Nini siri ya kilimo cha mpunga wilayani Bahi?

25 July 2023, 5:01 pm

Picha ni moja kati ya bwawa lililopo wilayani Bahi linalotumika kwa ajili ya kilimo cha mpunga. Picha na Fahari ya Dodoma.

Wakulima wa eneo hilo wanadai kuwa hawapendelei kutumia mbolea katika kilimo cha mpunga.

Na Yussuph Hassan.

Licha ya watu wengi kuamini kuwa mkoa wa Dodoma ni eneo kame lakini eneo hili linafaa pia kwa kilimo. Wakazi wa wialaya ya Bahi wamekuwa wakikitumia kipindi cha masika kwa kupanda mpunga ambapo maji ya mvua yanayo tuama katika mabwawa hutumika kwaajili ya kilimo hicho.