Dodoma FM

Madarasa mapya kupunguza msongamano wa wanafunzi Makulu

28 September 2023, 10:40 pm

Picha ni Muonekano wa shule hiyo ya msingi Makuli iliyopo Jijini Dodoma.Picha na George John.

Ujenzi wa Madarasa Matano katika shule ya Dodoma Makulu tayari umekamilika huku ushiriki wa wananchi katika ujenzi huo ukitajwa kuwa mkubwa.

Na Mindi Joseph.

Shilingi milion 100 zimetumika katika ujenzi wa madarasa 5 katika shule ya msingi Dodoma Makulu na kuondoa changamoto ya watoto kusoma kwa Msongamano.

Madarasa haya yatapungunguza wanafunzi kusoma kwa awamu kama ilivyokuwa awali wengine kusoma asubuhi wengine Mchana.

Diwani wa kata ya Dodoma makulu Fadhili Chibago amaesema shule hiyo kongwe ilikuwa na upungufu wa Madarasa.

Sauti ya Bw.Fadhili Chibago.
Diwani wa kata ya Dodoma makulu Fadhili Chibago .Mindi

Katika hatua nyingine ameomba kufanyika kwa ukarabati wa madarasa yaliyochakaa kwani yanahatarisha usalama wa wanafunzi.

Sauti ya Bw.Fadhili Chibago.