

26 May 2025, 1:01 pm
RC Queen amesisitiza kuwa malipo hayo ni haki yamsingi kwa watumishi hao na ni muhimu kwao kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.
Na Kitana Hamis.
Wauguzi mkoani Manyara wameiomba Serikali kuwalipa stahiki zao kwa wakati ili waweze kujikimu kimaisha ili kutoa huduma bora kwawananchi.
Wito huo umetolewa wakati wa hafla ya kula kiapo cha maadili ya kazi ikiwa ni siku ya Waunguzi Duniani katika mkoa wa Manyara ambapo wauguzi walisisitiza umuhimu wa kutambuliwa kwa mchango wao katika sekta ya afya.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Manyara,Mhe.Queen Sendiga,amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri zote mkoani humo kuhakikisha wanawalipa wauguzi stahiki zao kwamujibu wa sheria na taratibu za utumishi wa umma.