Dodoma FM
Dodoma FM
8 May 2026, 12:01

Hatua hiyo inaashiria mwanzo rasmi wa utekelezaji wa mradi huo muhimu kwa maendeleo ya wilaya hiyo.
Na Kitana Hamis.
Wakazi wa Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma wanatarajiwa kunufaika na huduma bora za usafiri kufuatia kusainiwa kwa mkataba wa ujenzi wa stendi mpya ya kisasa ya mabasi, utakao gharimu zaidi ya shilingi bilioni moja hadi kukamilika kwake.
Wilaya hiyo imeshuhudia hafla ya utiaji saini wa mkataba huo iliyofanyika hadharani, ikiwahusisha Halmashauri ya Wilaya ya Chemba pamoja na mkandarasi atakayetekeleza mradi huo.

Aidha, wananchi pamoja na wawekezaji wametakiwa kutumia fursa mbalimbali za kiuchumi zitakazojitokeza baada ya kukamilika kwa mradi huo, unaotarajiwa kuchochea maendeleo ya sekta ya usafiri na biashara katika eneo hilo.
Kwa upande wake mkandarasi wa mradi huo ameahidi kutekeleza kazi hiyo kwa ufanisi na kuikamilisha kwa wakati uliopangwa ili kuhakikisha wananchi wanaanza kunufaika na huduma hizo mapema iwezekanavyo.