Dodoma FM

Mradi wa HEAT-Mzumbe yaweka mkazo kwenye mitaala yote

4 August 2026, 17:16

Chuo kimeweka mkazo katika kuongeza kipengele cha amali kwenye mitaala yote. Picha na Anwary Shabani

Hatua hizo zinatarajiwa kuongeza ubora wa elimu inayotolewa na Chuo Kikuu cha Mzumbe na kuzalisha wahitimu wenye maarifa, ujuzi na uwezo wa kuchangia maendeleo ya taifa katika nyanja mbalimbali.

Na Anwary  Shabani.         

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa William Mwegoa, amesema kupitia mradi wa HEAT, chuo kimeweka mkazo katika kuongeza kipengele cha amali kwenye mitaala yote iliyofanyiwa mapitio ndani ya kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Ni katika Ofisi za Idara ya Habari – MAELEZO zilizopo Mtumba jijini Dodoma, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa William Mwegoa wakati akizungumza na waandishi wa habari, amesema kupitia mradi wa HEAT, chuo kimeweka mkazo katika kuongeza kipengele cha amali kwenye mitaala yote.

Profesa Mwegoa amesema hatua hiyo inalenga kuwaandaa vijana kuwa na kujiamini wanapoingia kwenye soko la ajira, huku pia wakihamasishwa kutumia maarifa yao kubuni ajira na kuanzisha shughuli zao za kiuchumi badala ya kutegemea kuajiriwa pekee.

Katika hatua nyingine, Profesa Mwegoa amesema chuo kinaendelea kuweka mikakati ya kukuza vipaji vya wanafunzi, kujenga uwezo wa watumishi, kuimarisha tafiti na ubunifu, pamoja na kubuni vyanzo mbadala vya mapato vitakavyosaidia maendeleo ya miundombinu na uwekezaji wa chuo.

Sauti na Anwary Shabani.