Dodoma FM

Wananchi watahadharishwa kuhusu mvua za El nino

29 September 2026, 17:17

Picha ni hali ya hewa iliyobadilika baada ya mvua kubwa kunyesha baadhi ya maeneo. Habari leo.

Kutokana na hali ya mvua za El nino zinazotarajiwa mwanzoni mwa mwezi wa kumi hadi wa kumi na moja wananchi wameshauriwa kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa huku wakitakiwa kuweka mazingira yao katika hali nzuri kwa kusafisha mitaro na kuziba mashimo yasiyo ya lazima katika mazingira.

Na Victor Chigwada.

Wakazi wa Kata ya Ihumwa, jijini Dodoma, wametakiwa kuchukua tahadhari dhidi ya mvua za El Niño zinazotarajiwa kunyesha kuanzia mwezi Novemba, kwa mujibu wa utabiri wa hali ya hewa.mvu

Diwani wa Kata ya Ihumwa, Edward Magawa, amewataka wananchi wanaoishi katika maeneo ya mabonde na mikondo ya maji kuhama mapema na kutafuta maeneo salama, ili kuepuka madhara yanayoweza kusababishwa na mvua hizo.

Baadhi ya wananchi wamesema wanaoishi mabondeni wanapaswa kuchukua hatua za kutafuta makazi salama, huku wakiiomba Serikali kuhakikisha miundombinu ya kupitisha maji ya mvua inakuwa imara na inafanya kazi ipasavyo.

Simulizi na Victor Chigwada.