Mtoto (5) amefariki dunia baada ya kutumbukia kisimani Mpwapwa
12 October 2026, 17:00

Jamii imetakiwa kuchukua tahadhari katika maeneo yenye visima vya maji, hususan vile vilivyochimbwa kienyeji, ili kuzuia matukio ya vifo katika jamii. huku wakitakiwa kivifukiaa au kuvifunika visimia hivyo kwaajili ya usalama wa watoto katika jamii.
Na Stephen Noel.
Mtoto mwenye umri wa miaka mitano, aliyefahamika kwa jina la Erick Ibrahimu, mkazi wa Kijiji cha Vighawe, Kitongoji cha Chinyika, Wilaya ya Mpwapwa, amefariki dunia baada ya kudumbukia kwenye kisima cha maji kilichochimbwa kienyeji.
Akizungumza, mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Isaya Madeje, amesema kuwa marehemu alikuwa akichota maji pamoja na wenzake nyumbani kwao, ndipo alipotokea kuteleza na kudumbukia ndani ya kisima hicho.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Chinyika, Emanuel Madelemo, ametoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha visima vya maji vinajengewa kingo imara na kuwekwa mifuniko salama ili kupunguza hatari za watoto na wanyama kudumbukia ndani yake.