Dodoma FM

Jamii yatakiwa kuthamini utu wa Binadamu

14 July 2026, 17:28

Picha ni baadhi ya wakazi na viongozi wa mtaa wa Mtaa wa Hazina Kata ya Vighawe.Picha na Stephen Noel.

Uongozi umesisitiza kuwa kila mwanadamu anastahili heshima na matunzo wakati wa uhai na hata baada ya kufariki.

Na Steven Noel

Uongozi wa Mtaa wa Hazina Kata ya Vighawe Wilaya ya Mpwapwa umeiomba jamii kuthamini utu wa mtu na kumpatia haki zake kwa mujibu wa Katiba bila kujali hali yake wala kipato chake.

Wito huo umetolewa na baadhi ya viongo wa mtaa huo pamoja na wananchi mara baada ya kushiriki zoezi la kujenga kaburi la Bw. Joseph Ngowi aliezikwa na kijiji hicho baada ya ndugu zake kukosekana .

Aidha viongozi hao wamewapongeza wananchi wa Mtaa wa Hazina  kwa kujitolea nguvu na kuchangia kuhakikisha kaburi hilo linapata hadhi.

Sauti ya Noel