Dodoma FM

Serikali kuendelea kushirikiana na wadau binafsi kuboresha elimu

11 October 2023, 9:43 am

Picha ni mkutano wa viongozi wa serikali na Wakuu wa shule  binafsi uliofanyika jijini Dodoma. Picha na Yussuph Hassan.

Serikali itaendelea kushirikiana kwa karibu na Taasisi binafsi katika kuboresha Mfumo wa Elimu nchini.

Na Thadei Tesha.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda  amesema Serikali itaendelea kushirikiana kwa karibu na Taasisi binafsi katika kuboresha Mfumo wa Elimu nchini.

Hayo ameyasema leo katika Mkutano wa Wakuu wa shule  binafsi katika kujadili masuala mbalimbali ya kuboresha na kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili hususani katika mfumo wa elimu nchini.

Sauti ya Prof. Adolf Mkenda .
Picha ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda akiongea katika mkutano huo .Picha na Yussuph Hassan.

Katika Mkutano huo ambao umehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi ,Vijana na Ajira Mhe, protabasi katambi na naibu waziri wa elimu Mh Omari Kipanga.

Awali akizungumza katika mkutano huo Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi vijana na ajira Mh Protabasi Katambi ambapo amesema   kuwa kupitia wizara ya vijana kazi na ajira wanao  wajibu wa kuhakikisha wanatoa kipaumbele hususani katika suala la malezi na makuzi kwa watoto na vijana.

Sauti ya Mh Protabasi Katambi
Picha ni Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi vijana na ajira Mh Protabasi Katambi akizungumza katika mkutano huo.Picha na Yussuph Hassan.

Kwa Upande wake Naibu waziri wa Elimu Mhe, Omari Kipanga ametumia fursa hiyo kuelezea wajibu wa serikali na taasisi binafsi katika kutoa elimu nchini.

Sauti ya Naibu waziri wa Elimu Mhe, Omari Kipanga