Dodoma FM

Wabunifu waiomba serikali kuendelea kuwawezesha

19 May 2022, 3:12 pm

Na;Mindi Joseph.

Wabunifu wameiomba serikali kuendelea kuwawezesha ili kuendeleza Bunifu zao kutoka hatua moja kwenda nyingine kwa maendeleo ya Taifa.

Taswira ya habari imezungumza na Mkufunzi wa mafunzo ya matengenzo ya ndege kutoka chuo cha taifa cha usafirishaji Juma Msofe ambaye yeye amebuni kifaa cha kuhamisha ndege kutoka sehemu moja kwenda nyingine ili kuzuia ajali za ndege ardhini.

Amesema serikali iendelee kuwawezesha ili kuhakikisha Bunifu zao wanaziendeleza kwani jamii ya sasa inaendana na teknolojia.

.

Kwa upande wake Gabriel Jeremia ambaye ni mhadisi wa mitambo kutoka chuo cha taifa cha usafirishaji ambapo awali walibuni gari inayotumia umeme na mwaka 2019 walishinda nafasi ya kwanza katika maonyesho ya kitaifa ya sanyansi Teknolojia na ubunifu.

.

Serikali imetenga shilingi Bilioni 1 kwa ajili ya kuwaendeleza wabunifu watakao tambuliwa kwa mwaka 2022 kupitia mashindano ya kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu MAKISATU.