Dodoma FM

UVCCM Bahi yahimiza wananchi kuendelea kushiriki miradi ya maendeleo

11 May 2023, 11:12 am

Ramadhani Idd – Kijana wa Ccm akishiriki nguvu kazi katika miradi inayoendelea kutekelezwa Wilayani Bahi. Picha na Bernad Magawa.

Katibu wa Jumuiya hiyo wilaya ya Bahi Fatuma sanda amesema miradi mikubwa iliyopelekwa wilayani humo ni fahari ya wananchi .

Na Bernad Magawa.

Jumuiya ya Vijana wa chama cha Mapinduzi wilaya ya Bahi imetoa wito kwa wananchi kushiriki kikamilifu katika nguvu kazi ili kuunga mkono juhudi za serikali katika miradi yote ya maendeleo iliyopelekwa na serikali wilayani humo na kuhakikisha inasimamiwa na kukamilika kwa wakati.

Katibu wa Jumuiya hiyo wilaya ya Bahi Fatuma sanda amesema miradi mikubwa iliyopelekwa wilayani humo ni fahari ya wananchi wa Bahi hivyo ni wajibu wao kuhakikisha wanashiriki kikamilifu kila mmoja katika nafasi yake.

 Aidha amemshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hasani kwa kupeleka miradi mingi wilayani humo na kusema kuwa vijana wa CCM watakuwa mstari wa mbele kujitoa katika nguvu kazi kuhakikisha miradi hiyo inakamilika.

Sauti ya Fatuma Sanda – Katibu UVCCM wilaya ya Bahi
Katibu wa UVCCM wilaya ya Bahi Fatuma Sanda akishiriki miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa Wilayani Bahi. Picha na Bernad Magawa.

Naye Mkuu wa kitengo cha elimu ya awali na msingi halmashauri ya wilaya ya Bahi Boniphace Wilson amesema jumla ya Bilion 1.5 zimetolewa na serikali kwaajili ya Miundombinu ya elimu ambayo inapaswa kukamilika mapema mwezi Juni mwaka huu na kueleza kuwa kukamilika kwa miradi hiyo kutapunguza utoro mashuleni.

Sauti ya Mkuu wa kitengo cha elimu ya awali na msingi halmashauri ya wilaya ya Bahi.