Dodoma FM

Vijana Bahi waomba kandarasi ili wajikwamue kimaisha

9 August 2023, 5:58 pm

Picha ni Baadhi ya vijana hao wakiwa katika karakana yao. Picha na Bernadi Magawa

Vijana hao wameanzisha karakana ndogo ya kutengeneza samani mbalimbali na kuwasaidia vijana hao kujipatia kipato.

Na Bernad Magawa .

Baadhi ya vijana waliojiajiri Wilayani Bahi Mkoani Dodoma wameiomba Serikali kuwaunga mkono kwa kuwapa kandarasi katika maeneo waliyobobea ili waweze kujikwamua.

Hayo yamesemwa na vijana wa kikundi cha Umonga Kata ya Kigwe Wilayani humo walioanzisha karakana ndogo ya kutengeneza samani mbalimbali na kuwasaidia vijana hao kujipatia kipato.

Akizungumza na kituo hiki kilipotembelea karakana hiyo Kiongozi wa kikundi hicho Edwald Kalani amemshukuru Mbunge wa Jimbo la Bahi Kenneth Nollo kwa Kuwapa kandarasi ya kutengeneza zaidi ya madawati 500 na kuwaomba viongozi wengine kuwaunga mkono .

Sauti ya Kiongozi wa kikundi.
Vijana hao wanajivunia kupata kadarasi ya kutengeneza madawati zaidi ya 500.Picha na Bernad Magawa.

Naye katibu wa itikadi na uenezi wa ccm kata ya kigwe Jonathan Matonya ambaye pia ni mmoja wa mafundi wanaofanya kazi katika karakana hiyo amewataka vijana kuwa waaminifu ili waweze kuaminiwa na watu mbalimbali.

Sauti ya katibu wa Itikadi na uenezi.

Kwa upande wao baadhi ya mafundi katika karakana hiyo wakazungumza namna wanavyonufaika na fursa mbalimbali zinazopelekwa katika kituo chao kutoka kwa viongozi mbalimbali.

Sauti za baadhi ya mafundi.