Dodoma FM

Wananchi watakiwa kufahamu umuhimu wa Parachichi

14 August 2023, 6:25 pm

Watumiaji wa Tunda hili wanadai kunufaika na ulaji wa parachichi .Picha na Vondt.net.

Kwa mujibu wa Jarida la Jumuiya ya Moyo la Amerika linaelezea kuwa  kula Parachichi kunaweza kupunguza hatari ya Ugonjwa wa Moyo na Mishipa kulingana na utafiti mpya uliochapishwa hivi karibuni.

Na Abraham Mtagwa.

Wananchi Jijini Dodoma wameshauriwa kuwa watumiaji wazuri wa tunda la Parachichi kwani lina faida nyingi kiafya.

Akizungumza na Taswira ya Habari leo, Bw.Stephano Daburu ambaye ni Mteknolojia na Mtaalamu wa Afya amesema kuwa, tunda la Parachichi ni moja ya matunda muhimu yenye kazi nyingi na faida kubwa katika mwili wa binadamu tofauti na mitazamo ya Watu wengi  .

Sauti ya Mtaalamu wa Afya.

Aidha Taswira ya Habari imezungumza na baadhi ya watumiaji wa Parachichi wanaoishi Jijini Dodoma ambao wamekiri kunufaika na tunda hilo huku wakibainisha matumizi mbalimbali na faida zake katika mwili wa Binadamu.

Sauti ya Watumiaji wa Parachichi (Wananchi).
kula Parachichi kunaweza kupunguza hatari ya Ugonjwa wa Moyo. Picha na facebook.

Vilevile tumezungumza na Baadhi ya Wafanyabiashara wa Parachichi katika soko kuu la Majengo  Jijini Dodoma, kujua hali ya soko la Parachichi  na muitikio wa wananchi  katika kununua tunda hilo.

Sauti ya Wafanyabiashara wa Parachichi.