Dodoma FM

Mkuu wa wilaya Kongwa awabana watendaji wa maji Mtanana

2 November 2023, 11:51 am

Picha ni Mkaguzi wa Ndani akiwasilisha ripoti ya maji kwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa. Picha na ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Kongwa.

Hivi karibuni kikao hicho kilifanyika katika kata ya mtanana hii ni baada ya  kubaini uwepo wa harufu ya Ubadhilifu wa Mapato yanayokusanywa kupitia Miradi ya Maji katika Kata hiyo hali iliyopelekea kushamiri kwa matumizi ya fedha mbichi.

Na Mariam Kasawa.

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Remidius Mwema amevitaka vyombo vya Watoa huduma za Maji Kata ya Mtanana kuwasilisha haraka Nyaraka mbalimbali za matumizi ya fedha.

Sauti za wajumbe wa kikao na Mkaguzi wa Ndani
Picha ni baadhi ya wajumbe na viongozi walio hudhuria kikao hicho.Picha na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.

Mapema akiwasilisha taarifa hiyo mbele ya Mkuu wa Wilaya kupitia kikao cha pamoja na viongozi mbalimbali na vyombo vya watoa huduma za Maji kutoka Kata ya Mtanana na kuhusisha Vijiji vya Chigwingwili, Ndalibo, Mtanana ‘A’ na Mtanana ‘B’ taarifa hiyo ilibainisha ukiukwaji wa kanuni zinazosimamia ukusanyaji wa Mapato .

Sauti ya Remidius Mwema.

Mhe. Mwema amewataka Viongozi wa Kata na Vijiji pamoja na Wataalamu wa RUWASA kutimiza wajibu wao na kubaini mapema uwepo wa Ubadhilifu wa namna hiyo na kuchukua hatua mapema.

Sauti ya Remidius Mwema.

Taarifa ya Mkaguzi imebaini Kamati hizo kufanya matumizi ya fedha tasilimu (Mbichi) kiasi cha Tsh. 13, 834,335  (Ambapo Kijiji cha Mtanana ‘A’ pekee ni Tsh. 11,030,785 na Tsh. 2,803,550 Kijiji cha Ndalibo), Aidha malipo ya kiasi cha Tsh. 7,752,000.00 yalikosa viambata, Stakabadhi za kukiri na Orodha za walipwaji zilizosainiwa, huku kiasi cha Tsh. 4,271,045.00 bakaa baada ya Matumizi ikiwa ni kiasi kilichopaswa kupelekwa Benki kwa kadri ya Nyaraka lakini hakikuwahi kupelekwa Benki.