Dodoma FM

Wanawake waaswa kutokukata tamaa mitazamo hasi

19 May 2021, 1:26 pm

Na; James Justine

Jamii imetakiwa kutokuwa na mitazamo hasi kwa mambo mbalimbali wanayoyafanya wanawake katika kujiletea maendeleo na Taifa kwa ujumla.

Akizungumza na Taswira ya habari mkurugenzi wa kikundi cha akinamama kinachojihusisha na kuwainua wanawake jijini Dodoma (WOMEN OF POWER)  Bi.Shemsa Rukubayunga amesema wanawake wanaweza kufanya mambo makubwa katika jamii lakini bado wamekuwa hawaaminiwi ikilinganishwa na wanaume.

Ameongeza kuwa tamaduni zetu ndio changamoto hali inayochangia kuleta mitazamo hasi kwa wanawake.

Naye mmoja wa wanawake jijini Dodoma Bi. Nzera Gabriel  amesema wanawake wengi wamekuwa wakikata tamaa mara baada ya kuambiwa hawawezi kuacha mambo mbalimbali wanayoyafanya katika jamii.

Mwanamke anaweza ni kauli ambayo imepewa nguvu sana kwa jamii ya  sasa ili kuwainua wanawake wanaweza bila kusikiliza maneno yanayo wakatisha tama na lengo ni kupata maendeleo na mitazamo tofauti kutoka kwa wanawake.