Dodoma FM

Wafanyabiashara wa Mchele Bahi walia kukosa soko la uhakika

24 January 2024, 11:55 pm

kukosekana kwa soko la uhakika la mchele wilayani Bahi imeelezwa kuwa ni moja ya sababu inayorudisha nyuma maendeleo ya wakulima. Picha na Google.

Mamlaka zinazohusika na suala hili zinatakiwa kuharakkisha upatikanaji wa huduma ya soko ili wakulima wa mpunga waweze kuuza mchele badala ya kuuza mpunga ambao wanaeleza kuwa faida yake ni ndogo.

Na Bernad  Magawa.

kukosekana kwa soko la uhakika la mchele wilayani Bahi imeelezwa kuwa ni moja ya sababu inayorudisha nyuma maendeleo ya wakulima wa mpunga  huku wafanyabiashara wa mchele wakilalamikia ugumu katika kutafuta masoko ya mchele ambao unazalishwa kwa wingi wilayani  Bahi.

Wanasema licha ya wilaya ya Bahi kuzalisha kwa wingi  mpunga kwenye ukanda huu wa kati,  lakini bado ukifika wilayani hapa kwa mara ya kwanza huwezi kuona kwa haraka kiashiria chochote cha uwepo wa zao hili kwa wingi   kwani hakuna soko rasmi kwa ajili ya kuuza na kununua  mchele,  isipokuwa ni kwenye mashine za kukoboa mpunga  ndipo walipojishikiza wafanyabiashara wa mchele.

Sauti za Wafanyabiashara,

Hali hii ya kukosekana kwa soko wilayani hapa inasababisha mchele kuuzwa kwa bei kubwa kama vile haulimwi hapa kwani wafanyabiashara wengi wamekuwa wakinunua mpunga na kuusafirisha maeneo mengine badala ya kuukoboa na kuuza mchele hapa  hali inayopelekea vijana wengi wanaojishughulisha na uuzaji wa mchele kukosa fursa.

Sauti za Wafanyabiashara,

Pamoja  juhudi za muda mrefu za serikali kuweka soko wilayani hapa  lakini bado juhudi hizo hazijazaa matunda hali inayopelekea wajasiliamali wakiwemo akina mama kuendelea kupaza zauti.

Sauti za akina mama wajasiriamali