Dodoma FM
Dodoma FM
16 April 2026, 3:57 pm

Wanafunzi wa vijiji hivyo hulazimika kutembea kilomita 20 kila siku hadi kufika mahali sekondari hiyo ilipo.
Na Victor Chigwada.
Imeelezwa kuwa mazingira ya kupanga vyumba kwa wanafunzi wa sekondari Mpwayungu kutokana na umbali wa shule si salama kwao hasa kwa wasichana.
Shule ya Sekondari Mpwayungu inakadiriwa kupokea wanafunzi kutoka vitongoji na vijiji vyote vinavyo kizunguka kijiji hicho wanafunzi wa vijiji hivyo hulazimika kutembea kilomita 20 kila siku hadi kufika mahali sekondari hiyo ilipo hali inayopelekea wazazi kulazimika kuwapangia vyumba watoto wao ili wawe karibu na shule.
Taswira ya habari imezungumza na Mwenyekiti wa Kijiji Cha Mpwayungu Bw.Festo Manjechi ambapo amesema kukosekana Kwa mabweni katika shule hiyo kumepelekea wanafunzi kupanga vyumba mitaani ili wawe karibu na shule hali inayopelekea watoto hao kukumbana na tabia hatarishi.
Nao baadhi ya wanafunzi wameiomba serikali kuwajengea mabweni shuleni hapo ili kupunguza tatizo la utoro na tabia hatarishi zinazo pelekea baadhi ya wanafunzi kukatisha masomo yao.
Baadhi ya wazazi wanasema ujenzi wa mabweni shuleni hapo utasaidia wanafunzi kufanya vizuri katika masomo yao na kuwaepusha na mazingira hatarishi.