Dodoma FM

Walimu wametakiwa kuzingatia kanuni na taratibu za adhabu shuleni

7 May 2026, 16:22

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi Prof. Riziki Shemdoe akizungumza katika mkutano wa wadau wa elimu uliofanyika jijini Dodoma. Picha na Anwary Shaban.

Kwa sasa mkoa wa Dodoma upo vizuri kitaaluma ambapo mwaka uliopita ulishika nafasi ya pili.

Na Anwary Shaban.

Walimu wametakiwa kufuata kanuni na taratibu za utoaji adhabu shuleni ili kupunguza wimbi la utoro kwa wanafanzi.

Hayo yamesemwa na waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Tamisemi Prof. Riziki Shemdoe alipo kuwa akizungumza katika mkutano wa wadau wa elimu uliofanyika jijini Dodoma mei 6 2026 amewataka walimu kuzingatia umri sahihi wa wanafunzi pindi wanapo toa adhabu shuleni.

Sauti ya Prof. Riziki Shemdoe.

Aidha amempongeza mkuu wa mkoa wa Dodoma  Mhe ,Rosemery Senyamule kwa kuwapeleka walimu walio fanya vizuri kwenda kujifunza mafunzo nje ya nchi akiwa jumuisha walimu 34 na Mafisa Elimu 2 walio kwenda korea kujifunza zaidi.

Sauti ya Prof. Riziki Shemdoe.
Picha ni mkutano wa wadau wa elimu uliofanyika jijini Dodoma mei 6 2026.Picha na Anwary Shaban.

Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe,Rosemery Senyamule amesema kwa sasa mkoa wa Dodoma upo vizuri kitaaluma ambapo mwaka uliopita ulishika nafasi yapili huku dhamira ya dhati ya mkoa ni kushika nafasi yakwanza kitaifa.

Sauti ya Mhe,Rosemery Senyamule .

Nae Mkuu wa wilaya ya Dodoma Alhaj Jabir Shekimweri amempongeza  Rais Samia Suluhu Hassan kwa mafanikio makubwa ambayo Tanzania imeendelea kuyapiga katika kukuza sekta ya elimu na kujiandaa kwa 2028 ambapo darasa la 6 na7 watahitimu kwa pamoja.

Sauti ya Alhaj Jabir Shekimweri.