Ushirikiano wa jamii na polisi wapunguza matukio ya uhalifu Chang’ombe
9 July 2026, 16:16

Kwa pamoja, Jeshi la Polisi na wananchi wanaendelea kuthibitisha kuwa ushirikiano ni silaha muhimu katika kupambana na uhalifu na kuhakikisha amani, usalama na maendeleo ya Mkoa wa Dodoma yanayo endelea kudumu.
Na Anwary Shaban.
Ushirikiano kati ya wananchi na Jeshi la Polisi umetajwa kuwa chachu ya kupungua kwa vitendo vya uhalifu katika baadhi ya maeneo jijini Dodoma.
Miongoni mwa mitaa hiyo inayo tajwa kupungua kwa vitendo vya uhalifu ni pamoja na mitaa ya Chang’ombe na Chamwino ambapo hatua hiyo imechangia kuimarika kwa ulinzi na usalama wa raia pamoja na mali zao.
Wakizungumza baadhi ya wakazi wa mitaa hiyo wamesema miaka kadhaa iliyopita walikuwa wakiishi kwa hofu kutokana na matukio ya ukabaji na wizi yaliyokuwa yakifanywa na vikundi vya wahalifu, hali iliyowafanya wengi kushindwa kutembea nyakati za usiku.
Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Nduka kata ya chamwino Mohaamed Pampai anaeleza sababu zilizo peleke kukithiri kwa vitendo vya uhalifu katika mitaa hiyo kipindi cha nyuma .
Akizungumzia mafanikio hayo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi wa jeshi la Polisi ACP Gallus Hyera, amesema Jeshi la Polisi limeendelea kuimarisha operesheni za kuwabaini, kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria wahalifu wote.