Dodoma FM
17 July 2026, 16:53

Watu hao wamekuwa wakibaguliwa na hata kuitwa majina yasiostahili.
Na Lilian Leopold.
Mitazamo hasi inayoendelea kuwepo katika baadhi ya jamii kuhusu watu wenye ualbino, ikiwemo kuwaita majina yasiyofaa, imetajwa kuendelea kuwaathiri kisaikolojia na kuathiri ustawi wao.
Jamii ya albino imekumbwa na unyanyapaa na hata wengi kuyapoteza maisha yao kwa watu wanaoamini kwamba sehemu za mwili za watu wenye ulemavu wa ngozi yaani albino zinaweza kuwapatia utajiri.