Wananchi Handali watakiwa kuhifadhi chakula baada ya mavuno
16 June 2026, 17:27

Wananchi wanashauriwa kudhibiti upotevu wa mazao baada ya mavuno na kuhifadhi chakula kwa uangalifu ikiwa ni pamoja na matumizi sahihi katika ngazi ya familia na kuepuka uharibifu ili kulinda usalama wa chakula .
Na Victor Chigwada.
Wito umetolewa Kwa wakazi wa Kijiji Cha Handali kuhakikisha wanatunza chakula wakati huu wa msimu wa mavuno na kuepuka kuuza mazao ovyo.
Haya yameelezwa na Afisa kilimo wa Kata ya Handali Bw.Daudi Kolokoni ambapo amesema ni vema wakulima kuanza zoezi la uvunaji wa mazao ili kuepukana na adha ya mazao kushambuliwa na wadudu pamoja na sumu kuvu.
Amesema baada ya zoezi la mavuno kutamatika wananchi hao wanapaswa kuhidhi mazao na kuepukana na matumizi yasiyo ya lazima hususani sherehe mbalimbali ikiwemo sherehe za jando ili kuepuka upungufu wa chakula kwa hapo baadae.
Kolokoni ameongeza kuwa msimu huu wakulima wa kijiji cha Handali wamefanikiwa kuvuna mavuno ya kutosha tofauti na miaka ya nyuma.
Baadhi ya vijana wameeleza kuwa msimu huu wa mavuno ni fursa tosha kwa vikundi vya vijana na hata mtu mmoja mmoja kuwekeza katika ununuzi wa mazao Kwa bei nafuu Kisha kupata faida nyakati za uhitaji wa chakula.