Dodoma FM

Bodaboda ni kundi lenye uhitaji mkubwa wa damu

18 December 2023, 9:20 pm

Picha ni Bodaboda wakipatiwa elimu ya usalama barabarani Picha na Seleman Kodima.

Elimu ya usalama barabarani kwa Bodaboda bado inaendelea jijini Dodoma huku ikigusa mambo mbalimbali ikiwemo uchangiaji damu, huduma ya kwanza na jamii na tayari elimu hii imekwisha wafikia bodaboda takribani 180.

Na Mariam Kasawa.

Vijana wametakiwa kutambua kuwa usalama barabarani ni jukumu la kila mtu hivyo wanapaswa kujilinda na kuwalinda wengine.

Zoezi la elimu ya usalama barabarani linaloendlea hapa jijini Dodoma linalotolewa na shirika lisilo la kiserikali linalo julikana kama AMEND leo wamejikita katika elimu ya uchangiaji damu hususani kwa bodadoda.

Elimu ya usalama barabarani na uchangiaji damu ina uhusiano gani huyu hapa Afisa muhamasishaji damu salama kanda ya kati Bw. Bernadino Medaa akieleza zaidi.

Sauti ya Bw. Bernadino Medaa .
Mahitaji ya Damu kwa bodaboda ni makubwa sana kutokana na ajali zinazo wakumba kila siku .Picha na Seleman Kodima.

Maafisa usafirishaji maarufu kama bodaboda ni kundi ambalo linatajwa kuwa na muamko mdogo zaidi wa kuchangia damu huku kundi hilo likihitaji damu mara kwa mara .

Ramadhani Nyanza mratibu wa miradi kutoka shirika la AMEND anasema mahitaji ya Damu kwa bodaboda ni makubwa sana kutokana na ajali zinazo wakumba kila siku hivyo wanapaswa kuchangia damu ili kumbupunguza uhitaji wa damu.

Sauti ya Ramadhani Nyanza.