Dodoma FM

Jumla ya wakulima 4,099 wanufaika na mradi wa kilimo himilivu cha zao la mtama.

2 August 2021, 12:37 pm

Na;Mindi Joseph.

Growing Rainfed Crops in Dryland Zones:

Jumla ya wakulima 4,099 kati yao asilimia 51 wanawake na 49 wanaume wamenufainka na Mradi wa kilimo himilivu cha zao la Mtama kutoka shirika la Farm Africa wilayani Kongwa Mkoani Dodoma mradi unaotekelezwa nchini Tanzania.

Katika wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma katika kijiji cha Chamae kata ya Hogoro wakulima wameanza kunufaika na zao la mtama kupitia kupata masoko ya uhakika ambapo mpaka sasa tani 125 zimeuzwa na wakulima 84 kupitia kampuni ya TBL na wakulima kuingiza kipato ghafi cha jumla shilingi 68,750,000/=.

Taswira ya habari imezungumza na Kedimoni Yohana Masikini mkazi wa Chamae na mwanakikundi wa kikundi cha Tumaini Mtama, ambapo ameomba Serikali na washirika wa maendeleo kuendelea kuboresha upatikanaji zaidi wa mbegu bora za Mtama ili kuwa uzalishaji wenye tija zaidi kwa msimu ujao wa 2021/2022.

Naye Judith Samweli mkulima na mwenyekiti wa kikundi cha Tumaini Mtama katika kijiji cha Chamae amelishukuru shirika la Farm Africa kwakuendelea kuwasaidia wakulima kuendeleza kilimo cha za Zao la mtama ambacho kinawasaidia zaidi kujikwamua kiuchumi kwa kuwa na uhakika wa chakula na kipato.

Kwa upande wake Afisa Mradi wa kilimo himilivu cha zao la Mtama kutoka shirika la Farm Africa Mradi katika wilaya ya Kongwa, amesema mpaka sasa wanufainka katika mradi huo ni wakulima 4,099 kati yao asilimia 51 ni wanawake na 49 ni wanaume.

Tanzania inatajwa kuwa nchi bora katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini, kwa kuzalisha mtama bora, hivyo ni vema wakulima wakatumia mwanya huo kukuza uchumi wao.