Dodoma FM

Mbunge wa jimbo la Bahi aahidi kukamilisha vyumba vya madarasa katika kata ya Mpalanga

20 July 2021, 12:37 pm

Na; Victor Chigwada.

Wananchi wa kata ya Mpalanga Wilaya ya Bahi wameishukuru serikali kupitia mbunge wa jimbo hilo Mh. Kenneth Nollo kwa kuwaahidi kukamilisha vyumba vya madarasa pamoja na ukarabati wa kisima cha maji.

Wakizungumza na taswira ya habari baadhi ya wananchi hao wamempongeza mbunge huyo kwa juhudi zake za kuwasaidia kutatua adha hiyo ambayo ilikuwa imewaelemea wananchi wa eneo hilo.

Mwenyekiti wa kijiji cha Chidilo Bw.Mnyukwa Sakaila amesema walikuwa na changamoto ya ukarabati wa bomba la maji kutumia mfumo wa sola pawa pamoja na maboma mawili yaliyokuwa hayajapauliwa lakini yote kaahidi kuyashughulikia.

Naye Diwani wa Kata ya Mpalanga Bw.Baraka Ndahani amekiri kuwa mbunge wao amewaahidi kuwapaulia shule shikizi huku akiwakabidhi kiasi cha fedha kwaajili ya mradi wa maji.

juhudi za wananchi katika kupambana na changamoto mbalimbali zimeendelea kuungwa mkono na viongozi wa serikali ili kuhakikisha jamii inapata huduma iliyo bora.