Dodoma FM

Uzalishaji wa maji Dodoma waongezeka kwa asilimia 6.3

28 February 2023, 4:58 pm

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule akizungumza katika kikao hicho . Picha na Seleman Kodima.

Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira imefanikiwa  kupunguza upotevu wa maji kutoka wastani wa asilimia 39.1 na kufika asilimia 28.3 Disemba  mwaka 2022.

Na Selemani Kodima .

Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira mkoani Dodoma DUWASA imetaja mafanikio yaliyopatikana kipindi cha Miaka miwili ya  ya serikali ya awamu ya sita ambapo ni pamoja na ongezeko la uzalishaji wa maji kutoka wastani wa lita milion 61.5  na kufika  lita milion 67.8 kwa siku.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi mtendaji wa DUWASA Mhandisi Aron Joseph wakati akizungumzia  mafanikio ya serikali ya awamu ya sita katika kipindi cha miaka miwili kwenye sekta ya maji jijini Dodoma   ambapo amesema miaka miwili ya serikali ya awamu ya sita wamefanikiwa kuongeza makusanyo ya maduhuli kutoka wastani wa shilingi bilion 1.6 na kufikia shilingi bilion 2.3

Sauti ya Mkurugenzi mtendaji wa DUWASA Mhandisi Aron Joseph .

Aidha Mhandisi Aron amesema DUWASA wameendelea kutafuta vyanzo vingine vya maji kwa kuchimba visima maeneo ya pembezoni ambapo tayari eneo la nzuguni  wamechimba visima vitano vyenye uwezo wa kuzalisha lita milioni 7.5  huku pia wakiendelea kufanya utafiti wa maji chini ya ardhi katika maeneo ya zuzu na Bihawana.

Sauti ya Mkurugenzi mtendaji wa DUWASA Mhandisi Aron Joseph .

Awali Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amesema kuwa ongezeko la uzalishaji wa  maji katika mkoa wa dodoma umepiga hatua kwa miaka miwili kutokana na kukamilika kwa miradi mkubwa ya maji iliyogharimu kiasi cha fedha bilion 9.14.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule.

Pamoja na hayo  licha ya ongezeko la watu katika  jiji la Dodoma ambapo sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 inakadiria kuwa na watu  765179  ambapo takribani asilimia 91 wanapata huduma ya maji safi na salama kwa njia ya mgao  huku amhitaji yakionesha kuwa  ni lita milion 133.4 kwa siku.