Dodoma FM

Wakulima wa zabibu waomba elimu ya kuongeza thamani zao hilo

26 April 2023, 3:54 pm

Zabibu kavu zikiwa zimepakiwa katika vifungashio maalum kwaajili ya kuuzwa. Picha na Thadey Tesha.

Zabibu huzalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo Mvinyo, Sharbati, jamu pamoja na nyingine nyingi lakini elimu ya kuongeza thamani zao hili bado ni ndogo sana kwa wakulima.

Na Thadei Tesha.

Baadhi ya wakazi wa jiji la Dodoma wameiomba serikali kuendelea kutoa elimu zaidi juu ya namna bora ya kuendesha kilimo cha zao la zabibu na kuongeza thamani zao hilo.

Dodoma Tv imefanya mahojiano na baadhi ya wakazi wa jiji la Dodoma ambapo wamesema kuwa pamoja na kuwa zao la zabibu linaweza kuzalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo mvinyo,jamu na kukaushwa kwa ajili ya juisi lakini bado wakulima wengi hawana elimu hiyo hivyo kuozea shambani puindi zinapokosa wateja.

Sauti za wananchi.
Zabibu pia hutumika kuzalisha mvinyo pale inapo ongezwa thamani. Picha na Thadey Tesha.

Tari ni miongoni mwa taasisi ambazo zimejikita kufanya tafiti katika mazao mbalimbali yanayolimwa hapa nchini pamoja na kutoa elimu kwa jamii Juu ya namna ya kuongeza thamani je ni kwa kiasi gani wanatoa elimu kwa wakulima juu ya suala hilo?

Sauti ya mtaalamu kutoka Tari.