Dodoma FM

Lishe duni yatajwa kuwa chanzo cha utapiamlo kwa watoto wa umri wa chini ya miezi 6

29 June 2022, 1:38 pm

Na;Mindi Joseph.

Ukosefu wa lishe bora kwa watoto wachanga chini ya miezi 6 umetajwa kuwa chanzo cha watoto kupata  utapiamlo.

Akizungumza na taswira ya habari Juma Swedi afisa lishe hospital ya Rufaa Mkoa wa  Dodoma amesema ukuaji wa mtoto una mahusiano makubwa na ulaji wa mama.

Ameongeza kuwa ulaja wa mama unachangia katika ukuaji wa mtoto jambo ambalo huongeza ufanisi kwa watoto katika maisha ya utu uzima.

.

Aidha amesema watoto wengi wanalazwa hospitali kutokana na utapiamlo hivyo ni jukumu la wazazi kuhakikisha wanazingatia Lishe bora ambayo itasaidia kuepukana na tatizo hilo.

.

Utafiti wa taasisi ya lishe na chakula nchini unaeleza  kuwa zaidi ya watoto milioni tatu( 3) wa Tanzania wenye umri chini ya miaka 2 wanapata utapiamlo  kutokana na kukosa chakula cha kutosha.