Dodoma FM

Mkuu Wa Wilaya ya Bahi Godwin Gondwe Ahidi Kuendeleza Mazuri

28 January 2023, 9:13 am

Na; Bernad Magawa.
Mkuu wa wilaya ya Bahi Godwin Gondwe ameahidi kuendeleza mazuri yote yaliyofanywa na aliyekuwa Mkuu wa wilaya hiyo Mwanahamisi Munkunda na kuwaahidi wananchi wa Bahi kufanya kazi kwa uwezo wake wote ili kuhakikisha kuwa wilaya hiyo inaendelea kuwa ya mfano.
Mheshimiwa Gondwe ameyasema hayo katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halashauri hiyo ikiwa ni muda mfupi baada ya kuwasili wilayani hapo na kukabidhiwa ofisi.
Akizungumza katika kikao hicho amewapongeza viongozi na wananchi kwa mafanikio makubwa katika idara ya elimu kwa kushika nafasi ya kumi kitaifa katika matokeo ya Darasa la saba mwaka 2022.

Kwa upande wake aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Bahi mheshimiwa Mwanahamisi Munkunda ambaye kwa sasa amehamishiwa Wilaya ya Kinondoni, akitoa neno la kuwaaga viongozi na wananchi wilayani humo amewashukuru kwa kumpa ushirikiano wa kutosha katika kipindi cha utumishi wake.
Pia amewaomba wananchi wa Bahi kuendelea kuwa na mshikamano ili waweze kuendeleza juhudiz zote zinazolenga kuwaletea maendeleo wanachi wa Bahi.