Dodoma FM

MEMKWA mkombozi kwa watoto Nagulo Bahi

8 November 2023, 3:35 pm

Picha ni Diwani wa kata ya Bahi Agostino Ndunnu akiongea na wananchi wa Nagulo Bahi. Picha na Mariam Kasawa.

Mpango wa Elimu ya Msingi kwa Watoto Walioikosa MEMKWA ni moja ya jitihada za kufikia malengo ya maendeleo  endelevu hasa Elimu bora.

Na Mariam Kasawa.

Wakazi wa mtaa wa Nagulo Bahi Kata ya Bahi wametakiwa kujitokeza kuwaandikisha watoto kwaajili ya maandalizi ya kujiunga na elimu ya msingi na elimu ya watu wazima (MEMKWA).

Dodoma fm imefika katika kijiji hicho na kuzungumza na wananchi waliofika katika mkutano wa kijiji ,wenye lengo la kujadili mambo mbalimbali ikiwemo ulinzi na usimamizi wa watoto katika jamii.

Bwana Rajabu Mohamed ni Mkazi wa Bahi na mdau wa elimu yeye anawahimiza wazazi kujitokeza kuwaandikisha shule watoto wote ikiwemo mabinti wenye umri wa miaka 15 ambao hawakupata elimu waandikishwe ili kupata elimu maalum.

Sauti ya Bw.Rajabu Mohamed.
Picha ni Baadhi ya viongozi walio hudhulia mkutano huo wa kijiji cha Nagulo.Picha na Mariam Kasawa.

Elimu jumuishi ni aina ya elimu inayowaweka pamoja watoto wenye mahitaji maalumu yanayoonekana na yasiyoonekana, ya muda mrefu ama ya muda mfupi, wenye ulemavu na wale wenye uwezo wa juu kiakili katika ufundishaji na ujifunzaji.

Katika kulitambua hilo huyu hapa Bi jane Mgidange Mratibu wa Elimu jumuishi kutoka shirika la FPCT akiwataka wazazi kujitokeza kuwaandikisha watoto.

Sauti ya Bi. Jane Mgidange.

Nae mwalimu mkuu wa shule yamsingi Nagulo Bahi Bw. Richard Killian akizungumza kwa niaba ya Mratibu elimu kata ya Bahi akawataka wazazi kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha watoto wao wanapata elimu.

Sauti ya Mwl. Richard Killian

Wazazi ambao wanawatoto walioshindwa kupata elimu ya msingi kutoka na changamoto mbalimbali wametakiwa kujitokeza kuwaandishi watoto  hao hususani mabinti ili waweze kupata elimu.