Dodoma FM

Mvua yaleta athari katika baadhi ya maeneo jijini Dodoma

6 December 2023, 12:41 pm

Picha ni Nyumba za mtaa wa Medeli zikiwa zimezingirwa na maji. Picha na Alfred Bulahya.

Tukio hilo limetokea Usiku wa Kumkia Disemba 5 baada ya Mvua kubwa kunyesha jijini Dodoma na kusababisha eneo hilo kujaa maji na kusababisha baadhi ya nyumba kubomoka.

Na Seleman Kodima.

Mtu mmoja amejeruhiwa huku Zaidi ya Nyuma Tano za Mtaa wa Medeli East kata ya Dodoma Makulu zikibomoka baada ya Mvua kubwa kunyesha usiku wa kumkia leo na kuacha baadhi ya kaya wakiwa hawana Makazi.

Baadhi ya wakazi wa eneo hilo ambao ni waathiriwa wa tukio hilo wakizungumza na Taswira ya Habari wameelezea hali ilivyokuwa wakati wakijiokoa na janga hilo na maombi yao kwa Halmashauri ya jiji la Dodoma

Sauti za wakazi wa eneo hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini Alhaji Jabiri Shekimweri ambaye alifikia katika maeneo hayo na kushuhudia hali ilivyo ,amewaagiza wakala wa barabara za mijini na Vijijini TARURA kuhakikisha wanahamisha maji yaliyozungumza makazi ya wananchi hao na kutengeneza mitaro yenye muelekeo wa kuyatoa maji katika eneo hilo.

Sauti ya Mh Jabir Shekimweri.
Picha ni Nyumba za mtaa wa Medeli zikiwa zimezingirwa na maji. Picha na Alfred Bulahya.

Nae Meneja  wa TARURA wilaya ya Dodoma  Emmanuel Mfinanga amesema wanatarajia kuanza kazi leo kwa ajili ya kuhakikisha athari hiyo haijitokezi tena kwa wananchi licha ya barabara kuwa kwenye matazamio.

Sauti ya Bw.Emmanuel Mfinanga.

Vilevile Taswira ya Habari Imezungumza na Diwani wa Kata ya Dodoma Makulu amewataka wananchi wa mtaa huo kuwa na subira wakati utatuzi ukiendelea kufanyika katika eneo hilo.

Sauti ya Diwani wa Kata ya Dodoma Makulu.