

5 May 2023, 4:38 pm
Baadhi ya wafanyabiashara wanasema kuwa viongozi hao wamekuwa wakiahidi kupatia ufumbuzi baadhi ya changamoto hizo bila ya kutekeleza ahadi hizo.
Na Thadei Tesha.
Baadhi ya wafanyabiashara wa matunda na mbogamboga katika soko la maisha plus jijini Dodoma wameiomba serikali kufanya marekebisho kwa haraka kwani ni muda mrefu umepita tangu kuahidiwa ujenzi huo.
Dodoma Tv imefika katika soko hilo na kuzungumza na baadhi ya wafanyabiashara ambapo wamesema kuwa ni zaidi ya miaka mitatu imepita tangu serikali kubomoa baadhi ya vibanda kwa ajili ya marekebisho lakini bado suala hilo halijafanyiwa kazi.
lakini je ni kwa kiasi gani wanaathirika kutokana na chanagamoto hiyo?