Dodoma FM

Serikali yawataka wamiliki na wasambazaji wa mifuko ya plastiki kujisajili

18 April 2023, 2:07 pm

Kiwanda cha kuzalisha mifuko ya plastic. Picha na Fred Cheti.

Hivi karibuni Baraza la uhifadhi na usimamizi wa Mazingira NEMC kupitia Mkurugenzi wake Mkuu Dkt Samuel Gwamaka lilitoa maelezekezo kwa wamiliki na wazalishaji wa mifuko ya plastiki nchini kuhakikisha wanajisajili.

Na Fred Cheti.

Serikali hivi karibuni kupitia baraza la hifadhi na usimamizi Mazingira nchini (NEMC) iliwataka wamiliki, wasambazaji na wauzaji wa mifuko ya plastiki kujisajili katika baraza hilo ili kukomesha matumizi yasiyo sahihi ya mifuko plastiki.

Kufuatia tamko hilo la serikali Dodoma Tv imezungumza na wananchi jijini Dodoma kujua jambo hilo litasaidia kwa kiasi gani kupunguza matumizi holela ya mifuko na wamekuwa na maoni tofauti juu ya jambo hilo.

Sauti za wananchi
Baraza la hifadhi na usimamizi Mazingira nchini (NEMC) likizungumza na wamiliki, wasambazaji na wauzaji wa mifuko ya plastiki . Picha na Fred Cheti.

Hivi karibuni Baraza la uhifadhi na usimamizi wa Mazingira NEMC kupitia Mkurugenzi wake Mkuu Dkt Samuel Gwamaka lilitoa maelezekezo kwa wamiliki na wazalishaji wa mifuko ya plastiki nchini kuhakikisha wanajisajili ili kuondoa changmoto za uchafuzi wa mazingira zinazotokana na mifuko ya plastiki.

Sauti Mkurugenzi Mkuu NEMC