Dodoma FM

Leo tunaangazia Wafanyakazi wa Nyumbani

12 December 2023, 9:17 pm

Picha ni mfanyakazi wa nyumbani akifanya usafi . Picha na UN News.

Baadhi ya wafanyakazi wa Nyumbani wamekuwa hawana uhuru na vipato vyao.

Na Mwandishi wetu.

Kufuatia kuwepo kwa wimbo la baadhi ya waajiri na wazazi wa wafanyakazi wa nyumbani kutokuwapa uhuru wa kipato wafanyakazi wao baadhi ya wananchi wametoa maoni yao juu ya suala hili .

Baadhi ya wakazi wa Ntube kata ya Nkuhungu wamesema ipo haja elimu juu ya umuhimu wa wafanyakazi hao kuwa huru na kipato chao iwafikie wazazi pamoja na waajiri .