Dodoma FM

Ulinzi umeimarishwa katika viwanja vya maonesho ya nanenane Dodoma

7 August 2026, 16:41

Ulinzi umeimarishwa kuelekea maonesho ya naenae ya 33 yanayoendele katika viwanja vya John malekela. Picha na mtandao.

Katika hatua nyingine, ACP Hyera amewataka wataalamu wa tiba asili kuacha kujihusisha na vitendo vya ramli chonganishi vinavyoweza kusababisha migogoro na kuvuruga amani katika jamii, akisisitiza kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kuchukua hatua dhidi ya vitendo vyovyote vinavyohatarisha usalama na utulivu wa wananchi.

Na Mwandishi wetu.           

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Gallus Hyera, amewahakikishia Watanzania wote wanaoshiriki Maonesho ya 33 ya Kimataifa ya Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Dkt. John Malecela, Nzuguni jijini Dodoma, kuwa hali ya ulinzi na usalama imeimarishwa na hakuna tishio lolote la kiusalama.

ACP Hyera amesema hayo Agosti 6, 2026, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea banda la Jeshi la Polisi katika maonesho hayo. Amesema askari wameimarisha ulinzi katika maeneo yote ya maonesho ili kuhakikisha washiriki na wananchi wanaotembelea maonesho wanaendelea na shughuli zao kwa amani na utulivu.

Aidha, amesema Jeshi la Polisi limetumia maonesho hayo kutoa elimu kwa wananchi kuhusu masuala mbalimbali ya usalama, ikiwemo makosa ya mitandao, wizi wa mifugo, huduma zinazotolewa na Dawati la Jinsia na Watoto pamoja na mbinu za kujikinga dhidi ya uhalifu.

Sauti na Mwandishi wetu.