Pombe na sigara zatajwa kuharibu maadili ya vijana mpwayungu
28 August 2026, 16:53

Na Victor Chigwada.
Mwenyekiti wa Kijiji Cha Mpwayungu Ndg.Festo Manjechi amekiri uwepo wa makundi ya vijana kuharibikiwa na starehe za unywaji wa pombe, Lakini tayari ameanza kuitisha vikao vya kundi hilo na kutoa elimu ya umuhimu wao katika jamii pamoja na kudhibiti ufunguaji wa vilabu vya pombe muda wa asubuhi.
Imeelezwa kuwa uwepo wa vijana wengi mtaani katika Kijiji Cha Mpwayungu wanao jihusisha na unywaji wa pombe na uvutaji wa sigara ni chanzo cha kuwa na jamii isiyo salama.
Baadhi ya wazazi wamesema maadili mema yanaanza na mzazi nyumbani kabla ya jamii nzima hivyo ni vema wazazi kuwalea vijana wao katika maadili mema.
Serikali za mitaa zimejipanga kuunda kamati za kuelimisha vijana kuepukana na vitendo vya hivyo visivyo kuwa na tija Kwa jamii na kizazi Cha baadae.