Dodoma FM

Vijana washauriwa kujikita Katika kilimo Biashara na kuachana na mikeka

6 May 2026, 16:35

Tafiti zinaonyesha upotevu wa mazao baada ya kuvuna  ni tatizo kubwa hasa katika nchi zinazoendelea.Picha na Steven Noel.

Tafiti zinaonyesha upotevu wa mazao baada ya kuvuna  ni tatizo kubwa hasa katika nchi zinazoendelea ambapo Kwa mazao ya nafaka (kama mahindi, mpunga, ngano): hupotea takribani asilimia 10% hadi 20% wakati kwa mavuno na mazao ya mbogamboga upotevu unaweza kufikia asilimia 30% hadi 50%.

Na Steven Noel.

Vijana wameshauriwa kujikita Katika  kilimo Biashara  na kuachana na tabia za kamali na kubeti mikeka Ili kuwa na uchumi endelevu na uhakika wa chakula.

Kauli hiyo imesemwa na baadhi ya vijana wa wilaya ya Mpwapwa walioshiriki Katika mafunzo ya kilimo Biashara yaliyo andaliwa na shirika la  LIKOTO  Llinajishughulisha na kilimo endelevu Kwa vijana .

Wakiongea na taswira ya habari vijana hao wamesema vijana wengi wanafikiri kazi ya kilimo ni kwaajili ya vijana ambao hawajasoma jambo ambalo si sahihi.

Nae mratibu wa Shirika la LIKOTO  bwana Godfrey Mwenda amesema mafunzo hayo yatawasaidia vijana kupata stadi za kilimo Biashara ambazo zitawawezesha kuinua kipato cha familia zao na Jamii Kwa ujumla

Wakulima wengi hupoteza mazao wakati wa kuvuna na kusafirisha kutoka shambani kupeleka Nyumbani.Picha na Steven Noel.

Bwana Mwenda amesema kutokana na uelewa mdogo  wa jamii kuhusu utunzaji na uvunaji wenye tija hupelekea wakulima kupoteza mazao Hadi asilimia 10 Hadi 30 ya mazao waliyo vuna.

Kwa upande wake Afisa kilimo wilaya ya Mpwapwa Muhandisi Anna Temba  amesema wakulima wengi hupoteza mazao wakati wa kuvuna na kusafirisha kutoka shambani kupeleka Nyumbani ,hivyo ametoa wito Kwa wakulima kufuata kanuni bora za uvunaji na utunzaji wa mazao Ili kuweza  kupata tija.

Sauti ya kina Noel.