Dodoma FM

Vikundi vya kijamii, polisi kushirikiana kufichua ukatili

17 July 2026, 15:32

Mwanamke anapojikwamua kiuchumi anakuwa na hatari ndogo ya kufanyiwa ukatili.Picha na Mtandao.

Washiriki wa kikundi hicho wameahidi kuendelea kufanya kazi na Polisi na viongozi wa jamii ili kuhakikisha Mpwapwa inakuwa salama kwa wanawake na watoto.

Na Stephen Noel.

Vikundi mbalimbali vya kijinsia vinavyoanzishwa kwenye jamii kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi vimetakiwa kusaidia kufichua vitendo vyote vya uharifu na ukatili wa kijinsia.

Rai hiyo imetolewa na Mchungaji Mariam Makasi ambaye pia ni Diwani wa Viti Maalum, alipokuwa akizungumza na kikundi cha akina mama cha Itambue Thamani yako cha mjini Mpwapwa.

Mchungaji Makasi amesema mara nyingi makundi yaliyo hatarini zaidi kufanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ni pamoja na wanawake na watoto.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kikundi hicho, Vailet Masasi amesema kikundi chao kipo tayari kushirikiana na Polisi kutoa elimu na kuelimisha jamii juu ya madhara ya ukatili.

Aidha, Ester Peter mkazi wa Mpwapwa amesema mwanamke anapojikwamua kiuchumi anakuwa na hatari ndogo ya kufanyiwa ukatili.

Sauti Noel kina.