Dodoma FM

Wamachinga waungana kudumisha amani

3 July 2026, 16:47

Biashara za wamachinga hutegemea mapato ya kila siku, hivyo uwepo wa mazingira ya amani na utulivu ni muhimu. Picha na Mtandao.

Ameongeza kuwa biashara za wamachinga hutegemea mapato ya kila siku, hivyo uwepo wa mazingira ya amani na utulivu ni muhimu ili kuwawezesha wafanyabiashara kuendelea na shughuli zao bila usumbufu na kuhakikisha uchumi wao unaendelea kukua.

Na Anwary Shabani.

Wafanyabishara wa soko la machinga jijini Dodoma wamesema wapo tayari kulinda amani kuepuka maandamano yoyote yanayo tishia amani ya nchi.

Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Soko la Machinga Complex jijini Dodoma, Marico Magale, ambapo amesema maandamano yoyote yanayokusudiwa kufanyika nchini yanapaswa kuzingatia sheria kwa kupata kibali kutoka serikalini.

Magale ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari, akieleza kuwa wafanyabiashara wa soko hilo wanaelewa umuhimu wa kudumisha amani na utulivu katika mazingira ya biashara zao.

Aidha amesema hawapo tayari kuona hali yoyote inayoweza kuvuruga shughuli zao za kila siku.

Sauti ya Marico Magale