Dodoma FM

Vijana watahiriwa mara mbili kiteto

3 August 2026, 11:51

Vitendo vya kikatili vinavyofanywa dhidi ya vijana katika jamii mkoani manyara vya kutahiri maramili. Picha na mtandao

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto amesema hakuna mtu aliye juu ya sheria, na vitendo vya ukatili vitachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Na Hamis Kitana.

Vitendo vya ukatili vinavyodaiwa kufanywa dhidi ya baadhi ya vijana  kwa kutairiwa mara ya pili, kwa madai ya kukiuka mila na tamaduni, vimeibua mjadala wilayani Kiteto mkoani Manyara.

Jumuiya ya Maridhiano na Amani kwa kushirikiana na Serikali imeanza kuwakutanisha pande husika ili kupata suluhisho la kudumu na kuzuia matukio hayo kuto kujirudia.

Wahanga wameomba jamii kutumia mazungumzo badala ya ukatili, huku viongozi wa mila wakisisitiza kuheshimu mila kwa kuzingatia sheria za nchi.

Sauti na Hamis Kitana.