Dodoma FM

Wanafunzi walalamika kutembea umbali mrefu

24 September 2026, 16:49

Picha ni wanafunzi wakitoka umbalimrefu kuelekea katika masomo shuleni. Picha na mwananchi.

Hatua hizo ni pamoja na kutenga eneo katika kitongoji cha Mbweko, pamoja na kuanzisha ujenzi wa shule katika kitongoji cha Ng’ambo kwa nguvu za wananchi, Ili kuwasaidie wanafunzikutokutumia muda mrefu wanapokuwa barabari katika kuhakikisha wanapata elimu bora bila changamoto yeyote.

Na Victor Chigwada.

Wakazi wa vitongoji vya Mbweko na Ng’ambo, Kata ya Mlowa Barabarani, wamelalamikia umbali mrefu wanaotembea watoto wao kwenda shule, wakisema hali hiyo inaweza kuathiri elimu na afya zao.

Wamesema changamoto hiyo inawaathiri zaidi wanafunzi wa madarasa ya chini, kutokana na kukosa uhakika wa usalama wanapokuwa njiani.

Kutokana na hali hiyo, wananchi wameanza kuchukua hatua za kuongeza shule shikizi ili kupunguza umbali wa safari kwa watoto hao, huku wakiomba Serikali kuunga mkono juhudi hizo.

Akizungumzia changamoto hiyo, Mwenyekiti wa Maendeleo wa Kata ya Mlowa Barabarani, Anjero Lukasi, amekiri uwepo wa tatizo hilo na kusema tayari wameanza kuchukua hatua za kulitatua.

Simulizi na Victor Chigwada