Dodoma FM

Kamati za ufuatiliaji kuchochea uwajibikaji kata ya Paranga Chemba

19 November 2026, 16:30

Picha ni baadhi ya baadhi ya wajumbe wakamati ya ufuatiliaji. Picha na Mariam Matundu.

Itakumbukwa kuwa serikali imeunda muongozo wa kitaifa wa ufuatiliaji na tathimini ya miradi na programu za maendeleo ili kuzuia miradi kutekelezwa chini ya kiwango, kuchelewa au kuongezeka gharama ili kuhakikisha thamani halisi ya fedha za umma.

Na Mariam Matundu.

Kamati za ufuatiliaji katika vijiji vya Sori na Kelema kuu kata ya Paranga wilayani Chemba zimetajwa kuchochea uwajibikaji katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika kata hiyo.

Hayo yameelezwa wakati wa mafunzo kwa kamati za ufuatiliaji katika kata hiyo yaliyotolewa na taasisi ya WAJIBU  wakishirikiana na taasisi ya AFNET kwa siku tatu kuanzia November 16 hadi 18 mwaka 2026.

Wakielezea ujenzi wa zahanati katika Kijiji cha Sori baadhi ya wajumbe wakamati ya ufuatiliaji wamesema kuwa wamefanya kazi kubwa ya kuhamasisha wananchi kuchangia ujenzi huo kwanguvu zao.

Picha ni baadhi ya baadhi ya wajumbe wakamati ya ufuatiliaji. Picha na Mariam Matundu.
Sauti za wajumbe Sori.

Licha ya wananchi kukamilisha jengo la zahanati katika ngazi ya lenta ni zaidi ya miaka 5 sasa hakuna hatua yoyote imechukuliwa na serikali katika kukamilisha jingo hilo.

Wakati huohuo kamati ya ufuatiliaji kwa kushirikiana na wananchi katika Kijiji cha kelema Kuu wamefanikiwa kujenga ofisi ya seriakali ya Kijiji na kufikisha katika nganzi ya lenta huku wakiomba serikali kukamilisha jingo hilo ili kurahisha huduma kwa wananchi.

Sauti za wajumbe kelema kuu.