Dodoma FM

Polisi waonya watu wanaotishia usalama wa wananchi Dodoma

16 October 2026, 16:25

Picha ni Mkuu wa Polisi Wilaya ya Dodoma Mjini, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Daudi Nkuba, akizungumza na wananchi. Picha kutoka Facebook.

Wananchi wamesisitizwa umuhimuwa wananchi kuzingatia usalama wao na usalama wa jamii wanazo toka kwa kutoa taarifa kwa wakati wanapo baini viashiria vya hatari, ili kusaidia kuzuia uhalifu na kuimarisha amani katika maeneo yao.

Na Anwary Shabani.

Mkuu wa Polisi Wilaya ya Dodoma Mjini, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Daudi Nkuba ametoa onyo kwa watu wanao jihusisha na vitendo vya kutishia na kuwatia hofu wananchi wengine watambue kuwa hakuna alie juu ya sheria hivyo atakae kiuka atachukulia hatua za kisheria.

Nkuba amesema hatua zimeanza kuchukuliwa dhidi ya watu wanao jihusisha na vitendo vya uhalifu na vitisho, huku akiwataka wananchi kushirikiana na vyombo vya usalama kwa kutoa taarifa za vitendo vinavyo hatarisha usalama katika maeneo yao.

Nae Diwani wa Kata ya Kiwanja cha ndege jijini Dodoma, Yona Isaya Lekele, amesema elimu ya usalama iliyo tolewa na Jeshi la Polisi katika mkutano huo itawasaidia wananchi kuongeza uelewa wa masuala ya usalama na kuchukua hatua za kulinda maisha yao, mali pamoja na shughuli zao za biashara.

Aidha, diwani huyo amewahimiza wananchi kuwa makini na kuchukua tahadhari wanapo baini vitendo vinavyo tia mashaka au hali zinazo weza kuhatarisha usalama, akiwataka kutoa taarifa kwa vyombo husika badala ya kuchukua  sheria mkononi.

Mkutano huo ni sehemu ya juhudi za kuimarisha ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na wananchi katika kupambana na uhalifu na kujenga mazingira salama kwa watu na shughuli zao za kiuchumi jijini Dodoma.

Simulizi na Anwary Shabani.