Migogoro ya kimahusiano ifanyiwe utatuzi mapema kuzuia mauaji
13 October 2026, 15:31

Katika kipindi cha hivi karibuni, taarifa za matukio ya mauaji yanayohusisha wenza na wanandoa zimeendelea kuibua maswali mazito miongoni mwa watanzania huku wivu wa kimapenzi, migogoro ya kifamilia, kutokuelewana na madai ya usaliti ni miongoni mwa sababu zinazotajwa katika baadhi ya matukio hayo.
Na Fred Cheti.
Wananchi wametakiwa kuchukua hatua za mapema katika kutatua migogoro ya kimahusiano na kutokufumbia macho vitendo vya vitisho na ukatili, kufuatia matukio ya mauaji yanayohusisha wanandoa na wapenzi yanayoendelea kuripotiwa nchini.
Nyumba inayopaswa kuwa mahali pa amani, upendo na usalama imeendelea kuhusishwa na matukio yanayogusa dhamiri za wengi, pale ambapo tofauti za kimahusiano zinapogeuka kuwa vitendo vya ukatili na wakati mwingine kusababisha vifo.
Wakizungumza na KM24 FM baadhi ya wananchi katika Manispaa ya Kahama wanaona hali hii kuwa ya kutia wasiwasi na wanatoa wito wa kuchukuliwa hatua za pamoja ili kuzuia migogoro ya kifamilia isigeuke chanzo cha kupoteza maisha.
Lakini je, nini kinaweza kumfanya mtu ashindwe kudhibiti hisia zake na kuchukua uamuzi unaoweza kugharimu maisha ya mwingine?
Ili kupata majibu, KM24 FM imezungumza na mwanasaikolojia ambaye ( JINA LA MWANASAIKOLOJI) anaeleza namna hali ya kisaikolojia na mwenendo wa mahusiano vinavyoweza kuchangia kuongezeka kwa migogoro.
Ambapo anaeleza umuhimu wa watu kujifunza kudhibiti hisia, kuwasiliana kwa heshima na kutafuta msaada wa kitaalamu pale wanapokabiliwa na migogoro inayojirudia.
Hata hivyo, je, Jeshi la Polisi lina ujumbe gani mahsusi kwa wananchi kuhusu namna ya kushughulikia migogoro inayohatarisha maisha?
Mfululizo wa matukio haya unatoa onyo kwamba migogoro isiyoshughulikiwa kwa njia salama inaweza kuwa na madhara makubwa. Lakini jambo la msingi ni kuelewa kuwa mauaji si suluhu ya mgogoro wowote, na hakuna tofauti ya kimahusiano inayoweza kuhalalisha kuchukua uhai wa mwingine