Dodoma FM

Zaidi ya watoto milioni 1.1 kupata chanjo ya polio awamu ya pili

28 September 2026, 16:50

Picha ni Dkt.Khatibu Kazungu katibu tawala wa mkoa wa Dodoma akizungumza kuhusu chanjo hiyo.Picha na Anwary Shaban.

Wazazi na walezi mkoani Dodoma wanakumbushwa kutokosa fursa hiyo, kwa kuhakikisha watoto wao wanapata chanjo katika kipindi hiki cha kampeni, kwa kuwa kinga ya mtoto ni jukumu la pamoja la familia na jamii.

Na Anwary Shaban.

Watoto zaidi ya milioni 1.1 mkoani Dodoma wanatarajiwa kupata chanjo ya matone ya polio katika awamu ya pili ya kampeni, huku wazazi na walezi wakitakiwa kuhakikisha watoto walio chini ya miaka 10,wakiwemo waliopata chanjo katika awamu ya kwanza wanapata Tena chanjo hiyo

Akizungumza jijini Dodoma DKt.Khatibu Kazungu ambaye ni katibu tawala wa mkoa wa Dodoma amesema utekelezaji wa kampeni utafanyika katika maeneo mbalimbali ikiwemo shule,vituo vya kutolea huduma za afya, nyumba za ibada na nyumba kwa nyumba.

Aidha amesema wazazi na walezi wametakiwa kuwa tayari kuwapokea watoa huduma na kuhakikisha watoto wote walio chini ya miaka 10 wanapatiwa chanjo hiyo bila kujali kama walishapata katika awamu ya kwanza.

Kwa upande wa Afisa program ya chanjo kutoka mpango wa Taifa ya chanjo Lotalis Norbert Gadau amesema kwa wale watoto ambao hawakupata chanjo awamu ya kwanza na wale walio zaliwa hivi karibuni basi wataweza kupata chanjo hiyo na kupata utaratibu wa namna ya kuendelea kupatiwa chanjo na kusema kuwa kampeni hizo huchukua takribani miaka 2 mpaka 3 na kuanza upya kampeni za chanjo.

Nae Mganga mkuu mkoa wa Dodoma Pro.Thomas Rutachunzibwa amesema kuwa chanjo hiyo itaanza kesho tarehe 29 mpka 2 mwezi wa kumi

Ikiwajumlisha na watoto walio zaliwa hivi karibuni.

Ripoti ya Anwary Shaban.